Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,UN wameunga mkono pendekezo la kuanza kutumika kwa Ndege maalum za upelelezi mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC ili kulinda usalama wa Raia.
Mkuu wa Operesheni za Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous amesema kuwa amewasilisha ombi maalumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha mpango wa kutumika kwa ndege maalumu zenye uwezo wa kuona hata wakati wa usiku kwenye maeneo ya Mashariki na Mpakani mwa DRC na Rwanda.
Pendekezo hilo
limepingwa vikali na nchi ya Rwanda, huku baadhi ya Mataifa yakionesha
wasiwasi wao iwapo ndege hizo zitaidhinishwa kutumika kuongezea nguvu
vikosi vya MONUSCO katika kuimarisha usalama nchini humo.
Iwapo Baraza la
Usalama litaidhinisha mpango huo itakuwa ni maraya kwanza kwa UN
kupitisha mpango kama huo nchini DRC mpango utakaosaidia pia kukabiliana
na Waasi.(CHANZO:RFI)
Post a Comment