Home » » JACK WA CHUZI, SKAINA NA BABY CANDY WAZIDI GOMBANIA PENZI LA TIMBULO

JACK WA CHUZI, SKAINA NA BABY CANDY WAZIDI GOMBANIA PENZI LA TIMBULO

Written By shebby on Tuesday, January 1, 2013 | 4:16 AM


http://www.bongocelebrity.com/wp-content/uploads/2012/05/Timbulo.jpgMASTAA wasichana wa mjini, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz, Skyner Ally ‘Skaina’ na Baby Candy wamejikuta wakirushiana matusi kupitia mtandao wa kijamii wa BBM kisa kikiwa ni msanii wa Bongo Fleva, Ally Timbulo.
Skyner Ally ‘Skaina’.
Katika sakata hilo, Jack Chuz alitajwa kuwa ndiye chanzo cha mabinti hao kugombana kwani mmoja alikuwa akimtetea shoga yake kwa kudai anataka kunyang’anywa bwana.
Aliyelianzisha bifu hilo ni msanii mmoja rafiki yao na akina Baby Candy (jina linahifadhiwa) ambaye alianza kwa kumtumia ujumbe wa matusi Skaina na kumwambia anaiba mabwana wa wenzake akimaanisha anataka kumuiba Timbulo.
Baada ya matusi kutua kwa Skaina aliyetuma ‘pini’ ya Timbulo mtandaoni akimuombea marafiki, Baby Candy naye aliamua kumtupia Skaina maneno makali akimalizia kwa kumwambia kuwa anaingilia vitu asivyovijua.
Ilifahamika kuwa baada ya kusoma ujumbe wa Baby Candy, Skaina alimporomoshea matusi mazito ambayo hayaandikiki akimalizia kwa kumwambia kuwa hana lolote bali anatafuta tu ustaa mtandaoni.

http://www.gushit.com/files/bookmark_photos/a7468b0461L.jpg
Hata hivyo, inaelezwa kuwa matusi hayo yalimkera Timbulo ambaye naye alijibu kupitia BBM akidai kuwa asingependa jina lake litumike vibaya kwani hana demu wala hawara kati yao hivyo anawaona kama machangu tu.
Akizungumzia ‘sheshe’ hilo, Baby Candy aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa anamshangaa Skaina kumtumia maneno makali kwani amemuona mjinga na hana muda wa kujibizana naye kwa sababu si mstaarabu.
Kwa upande wake Jack Chuz aliomba aachwe kwanza akiahidi kupiga simu kwa mwandishi wetu, jambo ambalo hakulifanya hadi gazeti hili linakwenda mitamboni.
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger