Home » » BONDIA WA TANZANIA ALIYEUAWA KWA KUCHINJWA HATIMAYE AZIKWA

BONDIA WA TANZANIA ALIYEUAWA KWA KUCHINJWA HATIMAYE AZIKWA

Written By shebby on Wednesday, January 9, 2013 | 12:57 AM



Mwili wa Dotto Kipenga ukiwa umebebwa tayari kwa mazishi.

MABONDIA na makocha wa mchezo huo wameonyesha huzuni zao kufuatia kifo cha bondia Dotto Kipenga, aliyefariki dunia usiku wa mkesha wa mwaka mpya Mburahati jijini Dar.
Kipenga alifariki dunia baada ya kuchinjwa na kijana asiyejulikana wakati akiwa baa akisherehekea mwaka mpya.
Wakizungumza na Championi Ijumaa, makocha na mabondia hao walisema kifo cha Kipenga kimeacha pigo kubwa katika mchezo wa ndondi nchini.
Kocha Rajabu Mhamila ‘Super D’ ndiye aliyeanza kufunua kinywa: “Alichofanyiwa ni unyama wa hali ya juu na hatukutegemea tukio kama hilo kutokea kwa kuwa dakika chache kabla ya kifo chake tulikuwa naye, ilipofika saa nane usiku tulishangazwa na taarifa ya kuchinjwa, jambo ambalo hatukuliamini.
“Amekufa kipindi ambacho alikuwa kocha wa ngumi katika Klabu ya Zugo iliyopo Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa akiwanoa vijana na siku ya tukio aliomba ruhusa ofisini kwake kwa ajili ya kwenda Mburahati kula sikukuuu na familia, ndipo lilipotokea tatizo hilo.”
Kipenga alizikwa Januari Mosi, mwaka huu kwenye makaburi ya Kigogo Mburahati jijini Dar.
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger