Home » , » CHECK OUT YANGA WAKIPIGA MAZOEZI UTURUKI

CHECK OUT YANGA WAKIPIGA MAZOEZI UTURUKI

Written By shebby on Monday, January 7, 2013 | 11:40 PM




Wachezaji wa Young Africans wakiwa katika mazoezi ya asubuhi leo hii - Antalya Uturuki
Wachezaji na bechi la ufundi la timu ya Young Africans wamefurahishwa na hali ya kambi hapa katika mji wa Antalya kwamba hali ya hewa ni nzuri, vyakula aina zote vinapatiikana na huduma za mazoezi kwa ajili ya kambi ni za kiwango cha juu sana.
Wakiongea na www.youngafricans.co.tz Kocha wa makipa Razaki Siwa amesema kw akeli hali ya hewa sio mbaya kama ilivyokuwa ikiripotiwa hapo awali, hali ya hewa ni nzuri, mazingira ya kambi ni ya kuridhisha vifaa vya kwa ajili ya mazoezi vipo kwa wingi hivyo inakuwa nio rahisi kwetu walimu kuwaelekeza wachezaji wafanye nini.
Kocha Siwa amesema pia wanaushukuru uongozi wa Young Africans kwa kuamua kuileta timu kambini nchini Uturuki kwani wachezaji wanapata nafasi nzuri ya kujifunza kwa pamoja, mafunzo ambayo hayana bughuza kwani kambi ipo katika hadhi ya kimataifa ndio maana timu nyingi za Ulaya


















Wachezaji wa Young Africans wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Fame Residence Analya - Uturuki





zinapenda kuja kuweka kambi eneo tulivu kama hili la Antalya.
Fred Felix Minizro kocha msaidizi kwa upande wake amesema hali ya kambi kwa ujumla ni nzuri, na kuhusu hali ya hewa ni baridi ya kisai tu kama Mbeya na Arusha hivyo haoni kama hali ya hewa inaweza kuwa ni kikwazo katika kambi hii ya mafunzo.
Naye kiungo mshambuliaji Saimon Msuva amesema wanafurahia kupata nafasi hii ya kuja kuweka kambi nchini Uturuki, kwani anaamin mazingira na huduma z akambi ni nzuri kabisa hivyo wanayapokea vizuri mafunzo ya kocha mkuu Brandts na pindi watakaporudi Tanzania wataweza kuwapa raha wapenzi wa soka kwa kuwaonyesha ni nini hasa wamekipata kwa kipindi cha wiki mbili.





















Magolikipa Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul wakiwa katika mazoezi ya asubuhi leo nchini Uturuki
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger