Akizungumza mara baada ya kipindi cha Maswali na Majibu, Spika MAKINDA amewataka Wabunge kubishana kwa hoja lengo likiwa ni kutimiza kazi iliyowaleta Bungeni ambayo ni kuwaletea wananchi maendeleo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia JANUARI MAKAMBA ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, amekerwa na tabia hiyo na anawakumbusha Wabunge wote kuwa lengo la kuanzishwa kwa vyama vya upinzani lilikuwa ni kuipa Serikali fikra mbadala katika Sera na kufuatilia maendeleo kwenye sekta kama vile Kilimo, Umeme, Maji, Afya,na elimu.
Hata hivyo Waziri MAKAMBA anatumia fursa hiyo kuhoji hotuba ya Mkuu wa Kambi Rasmi ya Ulinzani Bungeni kutogusia kabisa masuala hayo….
Akijibu baadhi ya Hoja za Wabunge kuhusiana na kutokuwepo kwa uwajibikaji na nidhamu ya fedha katika Halmashauri nchini Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa AGREY MWANRI amewataka Wabunge kushirikiana katika kutetea maslahi ya Wananchi.
Baada ya Bunge kushindwa kuhitimisha majadiliano ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bajeti hiyo zimehitimishwa jana kwa Waziri Mkuu MIZENGO PINDA kuzitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za Wabunge.
Post a Comment