Home » , » BAADA YA KUREKODI SAUTI YA WEMA NA KUISAMBAZA MTANDAONI, DIAMOND AFUNGUKA NA KULIONGELEA HILO

BAADA YA KUREKODI SAUTI YA WEMA NA KUISAMBAZA MTANDAONI, DIAMOND AFUNGUKA NA KULIONGELEA HILO

Written By shebby on Tuesday, April 23, 2013 | 8:34 AM



Skendo iliyokuwa ikiendelea mtaani kuhusu msanii Diamond na tuhuma za kumrekodi aliyekuwa mpenzi wake wa zamani mwanadada Wema Sepetu, msanii huyo amekir kuwa ni kweli alifanya tuhuma hizo kwaajili ya kulinda penzi lake.

 “Hivi karibuni Wema amekuwa akinipakazia mbovu kwa mpenzi wangu
Penny akiwa na leno la kutaka kuni haribia juu ya mimi na mpenzi wangu, nilichukia sana kwahiyo siku alivyoamua kunipigia simu ndipo niliamua kumrekodi ili kumsikilizisha Penny ambaye alikuwa haniamoni kabisa” Alifunguka Diamond.

Sauti hiyo ambayo ilitoka kwa Wema Sepetu ikiwa inambembeleza Diamond waweze kurudiana pamoja kwakuwa bado anampenda, Diamond amekiri kuirekodi hiyo sauti lakini amekana kuisambaza mitaani na hajui nani kafanya hivyo.

“Lengo langu kubwa ilikuwa ni kurekodi sauti hiyo  na kumsikilizisha Penny, sasa ambaye aliichukua na kuisambaza mitaani sijui ni nani, lakini hata mi sikujisikia vizuri nilipoisikia mitaani maana sikupenda hali iwe hivyo lakini ndo sina jinsi” aliongeza Diamond.

Baada ya kukiri kujutia, Diamond aliambiwa aombe msamaha Live ili Wema asikie ila alikataa na kusema hawezi kumuomba msamaha maana haoni kosa lake.
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger