Hiki ndicho kilichosababisha leotainmenttz iwe na mashaka na
kutoka kwa wimbo wake mpya wa “Mapenzi basi” uliopikwa katika studio za AM
Records, kutokana na interval ya muda kwa kuzingatia kuwa bado ‘ Ukimwona’
haina muda mrefu.
Leotaitainment imemtafuta Diamond Platinumz ambae alifunguka
kuwa wimbo huo ulivuja. Aliwalaumu sana AM Records na kwa kile alichodai kuwa
wanajua ni kwanini wao wameamua kuvuja wimbo huo japo wanakwepakwepa.
“AM record wenyewe sijui wanachonitafuta ni nini nikirekodi
nyimbo kwao wanakuwa wanazivujisha yani makusudi. ” Alifunguka Diamond.
Alisisitiza kuwa anajua AM Records ndio wako responsible kwa zoezi la kuvujisha
nyimbo zake, “yani ni wao mi najua kabisa ni wao, wanaongea ila wanakuwa kama
wanakwepakwepa ila mi najua kabisa ni wao.”
Huu sio wimbo wa kwanza kwa Diamond platinumz kuwa na
matatizo kutoka AM Records, ‘Ukimwona’ pia ni wimbo ambao ulivuja na ulipikwa
na AM Records, lakini Nataka kulewa iliyozua gumzo pia ilifanyika katika studio
hiyo hiyo chini ya producer Maneck.
‘Kesho hit maker’ amesema baada ya wimbo wake ‘Ukimwona’
kupigwa sana japo hakuitoa officially na imeshahit basi ameamua kuacha ipigwe
tu wakati anaangalia ngoma yake nyingine ya kuachia.
Leotainmenttz inaendelea kufanya jitihada za kumtafuta
Manecky wa AM Records ili kujua kwa upande wake nini kinatokea hadi nyimbo za
Diamond zinavuja kutoka katika studio hiyo.
Sikiliza Interview yote hapa
Post a Comment