Home » » CCM IMEWAPONGEZA VIONGOZI NA WAUMINI WA MADHEHEBU MBALIMBALI

CCM IMEWAPONGEZA VIONGOZI NA WAUMINI WA MADHEHEBU MBALIMBALI

Written By shebby on Thursday, May 16, 2013 | 6:49 AM

Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM imewapongeza viongozi na waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini hapa nchini, kwa kuwa wavumilivu na kujiepusha na vitendo vya uchochezi mara baada ya kutokea kwa mripuko wa Bomu katika kanisa la Mtakatifu JOSEPH jijini Arusha MAY 5 mwaka huu.
Akitoa taarifa Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kukamilika kwa mkutano wa kamati hiyo mjini Dodoma uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa CCM TAIFA Rais JAKAYA KIKWETE,Katibu wa Itikadi na uenezi NAPE NNAUYE amesema kitendo cha viongozi wa dini na waumini wao kuepuka uchochezi katika suala hilo kumesaidia kudumisha hali ya usalama na kuvirahisishia kazi vyombo vya usalama.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Taifa wa CCM,Rais JAKAYA KIKWETE anatarajia kukutana na wabunge wa chama hicho mjini Dodoma mwishoni mwa wiki hii, kujadili masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2010.
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger