Home » , » DAVID MOYES ASHINDWA KUKATAA KAMA MAN UNITED IMEINGIA KWENYE MBIO ZA KUMSAINI GARETH BALE.

DAVID MOYES ASHINDWA KUKATAA KAMA MAN UNITED IMEINGIA KWENYE MBIO ZA KUMSAINI GARETH BALE.

Written By shebby on Tuesday, August 27, 2013 | 4:30 AM



Boss wa Manchester United David Moyes amekataa kukanusha taarifa kwamba klabu yake imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya Gareth Bale baada ya kuibuka taarifa kwamba kuna imeibuka kushindana na Real Madrid katika mbio za kumsaini winga huyo wa Tottenham - huku ikiripotiwa kwamba Real wametoa ofa ya £86m ambayo Spurs bado hawajaikubali.

Wakati alipoulizwa kama klabu yake imeingia kwenye kinyang'anyiro cha saini ya Bale, Moyes alisema: "Nilisema tangu mwanzo nilipopewa hii kazi kwamba Manchester United itakuwa inajaribu kusajili wachezaji bora na bado tunajaribu kuiboresha timu yetu."

Akiongea baada ya sare ya  0-0 dhidi ya Chelsea, aliongeza: "Wamiliki wa timu wamenipa kila nafasi ya kumsajili mchezaji yoyote ninayemtaka na nataka kuendelea kutafuta wachezaji wa kuiboresha timu.

Hata hivyo bado Real Madrid inapewa nafasi kubwa ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales. 


Kocha msaidizi wa zamani wa United Mike Phelan, ameiambia  BBC Radio 5 live kwamba anategemewa Bale atajiunga na Madrid. 
"Nitashangazwa sana ikiwa Bale hatojiunga na Real Madrid siku chache zijazo. 
"Man United wangekuwa kwenye nafasi nzuri ya kumsajili kama wangetaka. Na itakuwa jambo la kusitikitisha kwa Bale kama hatohama Spurs kwenda Madrid.."
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger