Home » , » JOSE MOURINHO:"TUTATUMA OFA NYINGINE KWA UNITED KUMSAJILI ROONEY" - UNITED YARIPOTIWA KUWA TAYARI KUMUUZA LAKINI DILI LAZIMA LIMHUSISHE MATA

JOSE MOURINHO:"TUTATUMA OFA NYINGINE KWA UNITED KUMSAJILI ROONEY" - UNITED YARIPOTIWA KUWA TAYARI KUMUUZA LAKINI DILI LAZIMA LIMHUSISHE MATA

Written By shebby on Thursday, August 22, 2013 | 5:39 AM


Jose Mourinho amethibitisha kwamba Chelsea kwa sasa watasitisha mbio zao za kumuwania mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney mpaka klabu hiyo itakapocheza na United kwenye dimba la Old Trafford siku ya jumatatu.

The Blues wameshuhudia ofa zao mbili zikikataliwa na mabingwa wa premier league, huku kocha David Moyes akisisitiza kwamba mshambuliaji huyo wa England hauzwi.
 

Jana jumatano zilitoka taarifa kwamba United wapo tayari kuzungumza na Chelsea katika dili la uhamisho wa Rooney lakini ikiwa tu litamhusisha Juan Mata - lakini Mourinho amesema hakuna mazungumzo yatakayofanyika mpaka baada ya mechi ya jumatatu.

"Tulituma ofa kwa ajili [Rooney] huko nyuma na tutfanya hivyo tena baadae," kocha huyo wa kireno aliwaambia waandishi wa habari baada ya ushindi wa 2-1 dhidi Aston Villa.

"Lakini sitaki Chelsea ifanye kitu chochote kabla ya mechi ya Jumatatu tutakapoenda Old Trafford."
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger