Milovan ang'ata meno kwa Nyosso
KOCHA Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic ameshangazwa na kiwango cha beki wake, Juma Nyosso kutokana na jinsi kilivyoimarika na kutamka ni zaidi ya msimu uliopita, huku mchezaji huyo akimjibu: "Ni matizi tu." Nyosso nusura atemwe msimu huu wakati wa usajili kwa madai kuwa kiwango chake kiliporomoka huku mashabiki wakimzomea na kumwona hana maana. Beki huyo ameibuka ghafla na kucheza kiwango cha juu katika mechi za kirafiki na kuwafunika wageni Mkenya Pascal Ochieng na Komanbill Keita wa Mali ambao Milovan amesisitiza kuwa ni wazuri lakini wanahitaji kupewa muda. "Nimeshangazwa na kiwango cha Nyosso kwa sasa alivyocheza katika mechi za kirafiki za msimu huu, kiwango chake kimeimarika tofauti kabisa na ilivyokuwa msimu uliopita," alisema Milovan. "Nyosso wa msimu uliopita hakuwa makini, alikuwa anafanya makosa ya mara kwa mara katika uchezaji wake, lakini sasa hali ile haipo tena, ameimarika na anacheza vizuri na kwa kujituma," alisifu Milovan ambaye awali aliiambia Mwanaspoti jijini Arusha kwamba anataka ukuta imara kwa kuwatumia Keita na Ochieng kutokana na ufanisi wa wachezaji hao kwenye mechi za kirafiki za Arusha dhidi ya Mathare, Oljoro JKT na Sony Sugar. Lakini mabeki hao wa kigeni walipotua Dar es Salaam kwenye mechi mbili dhidi ya Sofapaka na Azam wakachemsha, akabadilisha mawazo na kumrudia Nyosso kundini. Hata hivyo, Nyosso alisema amefanya maandalizi mazuri ya kujiweka fiti. Ushindani wa namba katika beki ya kati umeongezeka kwani kombinesheni ya Nyosso na kiraka Shomari Kapombe inaonekana kufanya vizuri ingawa Keita na Ochieng nao kwenye mechi tatu za Arusha walianza vizuri. Beki wengine ni Hassan Khatib na Obadia Mungusa. ....... |
Sunzu akomba fedha zote za ubingwa
![]() |
Straika wa Simba, Mzambia Felix Sunzu. |
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom imeingia mkataba wa miaka mitatu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wa kudhamini ligi hiyo ikiwa imepanga kutumia kiasi cha Sh 1.7 bilioni.
Mshindi wa pili wa ligi hiyo atajizolea, Sh 50 milioni wakati Sh 30 milioni zitakwenda kwa mshindi wa tatu.
Sunzu analipwa Dola 3,500 kwa mwezi ambazo ni sawa na Sh 5.4 milioni ambazo ukizidisha kwa miezi 12 anapata Sh 65.1 milioni na ukiongeza na posho za mechi na gharama ndogondogo ambazo klabu inaingia, zinazidi Sh 70 milioni za bingwa wa ligi.
Klabu zimekuwa zikilalamikia ufinyu wa zawadi huku TFF ikitangaza kwamba mkataba mpya na mdhamini umeshasainiwa ingawa hakuna picha zozote za ushahidi zilizoonyesha wahusika wakianguka wino.
Ligi Kuu inashirikisha timu 14 ambazo zitacheza mechi 26 kuzunguka mikoa mbalimbali kila timu ikiwa na usajili wa wachezaji wasiopungua 25.
Huku udhamini wa Tanzania ukiwa kiduchu huko Afrika Kusini ambako kampuni za huko zimewekeza Tanzania katika sekta za madini, fedha na mawasiliano zinatoa zawadi za kufa mtu.
Mathalan bingwa wa Ligi Kuu Afrika Kusini inayodhaminiwa na Benki ya ABSA, ambayo ina hisa kubwa katika Benki ya Biashara ya Tanzania (NBC), bingwa anaondoka na kiasi cha Sh 1.9 bilioni.
Mshindi wa pili wa ligi hiyo anaondoka na kiasi cha Sh 926 milioni huku mshindi wa tatu akiweka kibindoni Sh 370 milioni.
Kinachoshangaza ni kuwa kampuni za kigeni zilizowekeza nchini zinamwaga mamilioni huko makwao lakini linapokuja suala la kudhamini michezo ya Tanzania, zinatoa zawadi ndogo wakati wanafaidi rasilimali mbalimbali kupitia uwekezaji wao.
Post a Comment