Home » » umati wa watu wafurika kusikiliza rufaa ya lema

umati wa watu wafurika kusikiliza rufaa ya lema

Written By shebby on Saturday, September 22, 2012 | 12:56 PM



umati wa watu wafurika kusikiliza rufaa ya lema

WAFUASI WA CHADEMA
Kesi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Ndugu 'Godbless Lema' imesikilizwa mapema leo Septemba 20 kwenye mahakama ya rufani jijini Arusha na jaji mkuu 'Othman Chande'. Kesi hiyo iliyofunguliwa na Mbunge huyo kupinga kutenguliwa kwake ubunge na mahakama kuu ilisikilizwa kwa takribani saa 2 kabla ya kuahirishwa ambapo 'Lema' aliwasilisha mahakamani hapo hoja 18 za kupinga hukumu ya awali ya kesi yake.
Ilifahamika hata kabla ya kesi
hiyo kusikilizwa mawakili wa pande zote mbili (Chadema na Ccm) waliandika barua zilizofika mahakamni hapo kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo kutokana na mawakili 'Tundu Lissu' anayemtetea Lema na kaka yake 'Alute Mughwai' anayewatetea walalamikaji kufiwa na baba yao mzazi. Kesi hiyo ambayo ilihudhuriwa na wafuasi wengi wa chama cha Chadema waliomsindikiza 'Lema' imeahirishwa hadi tarehe 2 Oktoba mwaka huu itakaposikilizwa tena.
 
'Lema' akiwasili mahakamani,


 
Askari polisi wakidumisha usalama maeneo ya Arusha wakati wafuasi wakimsindikiza Lema,
Umati wa wakazi wa Arusha waliofika eneo la Mahakama Kuu kusikiliza rufaa hiyo.
Wananchi wakiwa nje ya ofisi ya chama wanamsikiliza lema.
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger