

Baada ya maneno ya muda mrefu hatimaye usiku huu ukweli umejulikana kuwa
nani mbabe kati ya Man U na Real Madrid. Wababe hawa wamekutana katika
mechi ya marudiano iliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford na Man U
kuambulia kipigo cha goli mbili moja na kuwa ndiomwisho wa safari yao
katika kombe la UEFA, Real madrid wamefanikiwa kutinga robo finali kwa
jumla ya magoli 3-2.

Toka
mwanzo kabla mechi haijaanza kocha wa Man U Sir Alex Ferguson
alionyesha wasiwasi kuwa huenda akachezea kipigo kutokana na kauli
mbalimbali alizokuwa akizitoa kwa vyombo vya habari juu ya uwezo wa
mchezaji CR na jinsi gani anavyomhofia..........Poleni sana mashabiki wa
Man united but ndio mchezo huo. Jose Morinho ameonyesha kuwa kweli ni
kocha bora baada ya kuwachapa miamba hao wa Uingereza.
Post a Comment