Home » , » MARTIN KADINDA AWACHAMBUA DADA WA WEMA SEPETU

MARTIN KADINDA AWACHAMBUA DADA WA WEMA SEPETU

Written By shebby on Monday, March 18, 2013 | 8:38 AM

Huenda umekuwa ukimsoma tu msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Isack Sepetu bila kujua kuwa ana dada zake ambao wamesimama kimaisha licha ya kwamba si watu wa kuonekana kwenye vyombo vya habari mara kwa mara.
Juzikati, mwanamitindo maarufu wa kiume Bongo, Martin Kadinda kupitia blog yake ya mvutokwanza amewachambua dada watatu wa Wema huku akianika tabia zao kwa jinsi yeye anavyowafahamu kama anavyowaelezea hapa chini;
TUNU: Napenda kumuita The Perfectionalist. Huyu ni mama wa mtoto mmoja, anaishi nchini Marekani. Ni mpole na anapenda kusikiliza watu. Anapenda kuchukua muda kabla ya kutoa maamuzi ya jambo analopenda. Ni mtafutaji na amekuwa akiniita baby.
SUNNA: Huyu ana visirani kama mdogo wake Wema. Anaishi Marekani. Nampenda sana, ni mcheshi na napenda kumuita majimaji kwani anapenda sana kula…yeye ni bata ndefu kwa kwenda mbele.
Ni mpenzi wa fasheni na vitu asilia.
NURU: Ni mama wa watoto watatu, ameolewa na anaishi Dar. Napenda kumuita kubwa la maadui kwani hakuna kinachoshindikana kwake.
Tatizo lolote litakalotokea katika familia yake akionekana tu kila kitu kinakwenda sawa.
Ana ubavu wa kukontroo mambo
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger