Home » » DUDU BAYA BIASHARA ZIMENIWEKA NJE YA GAME

DUDU BAYA BIASHARA ZIMENIWEKA NJE YA GAME

Written By shebby on Friday, April 5, 2013 | 12:31 PM

Moja ya wasanii ambao waliwahi kufanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya nchini, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya, amesema kuwa alikuwa kimya kwa sababu alikuwa amebanwa na biashara nje ya mkoa wa Dar es salaam.
Dudubaya alisema kuwa mbali na muziki kuna vitu alikuwa akifanya ambavyo aliona kuwa hawezi kuvifanya huku anafanya muziki.
Akiongea kwa njia ya simu kutoka Mwanza, Dudubaya aliyewahi kutamba na nyimbo kama 'Nakupenda', 'Ruka Ruka', 'Mwanangu huna Nidhamu' alisema biashara anazofanya ambazo hakuwa tayari 
 


kuzitaja, zinamfanya asafiri sana mikoani na muda mwingi anakuwa Mwanza kwa sababu ndo kituo kikubwa cha biashara hizo.
Dudubaya alikanusha taarifa ambazo ziliwahi kusambaa kwenye mitandao ya jamii kuwa bado anaendelea na tabia yake ya ugomvi na akiwa Mwanza aliwahi kumpiga mtangazaji wa kituo kimoja mkoani humo.
"Niko kwenye muziki toka mwaka 1997, sijawahi kumpiga mtangazaji yeyote.Kuna hata baadhi ya waandishi wa habari walikuwa wanaandika skendo ambazo hazikuwa za kweli lakini sikuwahi mpiga yeyote wakati wengine nawajua.Nawaheshimu sana watangazaji, MaDj na waandishi wa habari, mimi siku hizi sio mgomvi tena kama zamani", alieleza Dudubaya.
Aliendelea kueleza kuwa kilichopelekea habari kusambaa kuwa kapiga mtangazaji ni mambo ya tofauti binafsi huko Mwanza na wala si ya kimuziki kama ambavyo habari zilisambaa.
Dudubaya anasema kwa muda ambao alikuwa kimya alikuwa akifikiria afanye muziki wa aina gani ili aweze kuwateka mashabiki wake kama ilivyokuwa awali.
Wimbo wa mwisho Dudubaya kutoa ilikuwa ni Mwaka 2011 ulikuwa unaitwa 'Mdundo'. Alisema mwaka 2013 amerudi rasmi kwenye na wimbo wake mpya utatoka mwishoni mwa wiki hii. Wimbo huo umerekodiwa hukohuko Mwanza katika studio inayoitwa One Love FX chini ya produza Tiddy Hotter.
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger