Katibu Mkuu wa klhttp://www.blogger.com/blogger.g?blogID=1052547122364561011#editor/target=post;postID=2778911938202018370abu ya Young Africans Lawrence Mwalusako leo
amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa
ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani kufuatia ku
malizika kwa mkataba wake wa miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako amesema
Ngasa amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda mrefu
kabla ya kuhamia katika timu ya Azam FC ambako alitumikia mkataba wa
miaka 3 uliomalizika mwisho mwa msimu huu.
Naye mwenyekiti wa mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb
amesema anashukuru kwa Ngasa kuamua kurudi nyumbani, kwani amekuwa
mchezaji anayejitolea kwa moyo wake wote katika timu zake zote
alizokuwa akichezea hali iliyompelekea kuendelea kuwa katika kiwango
cha hali ya juu.
Kwa kweli mimi binafsi nimefurahi kijana kurejea nyumbani, amerejea
katika timu inayomjali, inamsikiliza alisema Bin Kleb huku akimalizia
kwa kusema kuwa Ngasa ataitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka 2.
Aidha Ngasa mwenyewe amewashakuru wapenzi, washabiki na wanachama wa
klabu ya Yanga kuwa naye kwa nyakati zote, nilipohamia Azam walikua
wakishangilia, nilipohamia Simba pia walikuwa wakinipa moyo na
kunishangilia pia.
Nimeamua kurudi katika timu yanga ya zamani sababu ndio sehemu pekee
wanaponisikiliza na kunithamini, timu niliyotoka pamoja na kucheza kwa
moyo wangu wote bado viongozi wake hawakua na imani na mimi hicho ndo
kilichonipelekea kurudi katika timu yangu ya Yanga.
Ngsa anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu ya Yanga kwa ajili
ya kuongeza nguvu katika kikosi kitachoitumikia Yanga katika msimu ujao.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO (DMNM)
EVER FORWARD BACKWARD NEVER (EFBN)
Mrisho Ngasa akikabidhiwa jezi ya klabu ya Yanga na katibu mkuu Lawrence Mwalusako
Post a Comment