Home » , » RONALDO ANAMATUMAINI YA KUJUMUISHA KATIKA KOMBE LADUNIA

RONALDO ANAMATUMAINI YA KUJUMUISHA KATIKA KOMBE LADUNIA

Written By shebby on Friday, May 17, 2013 | 3:24 AM


RONALDO NA MATUMAINI YAKE.

                   BY SHEBBY




Ronaldinho bado hajakata tamaa ya kuchezea Brazil katika Kombe la Dunia 2014 licha ya kutojumuishwa katika kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki Kombe la Confederations.
Ronaldinho amekuwa akitamba sana Brazil na alipigiwa upatu kujumuishwa katika timu hiyo, lakini kocha Luiz Felipe Scolari aliamua kuacha nyota huyo aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa Fifa wa mwaka mara mbili nje ya orodha ya wachezai 23 walioteuliwa kushiriki dimba hilo la kujipasha moto litakaloanza Juni 15.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alikiri kuwa alishangazwa sana na kuachwa nje kwake, lakini bado ana matumaini kwamba ataitwa tena kujiunga na timu kabla ya Kombe la Dunia 2014 litakaloandaliwa na Brazil.
“Nilitaka sana kuwa katika orodha na nilikuwa na matumaini, lakini hili halikufanyika nilivyopenda," Ronaldinho alisema. “Lakini hili linanitia motisha kujaribu hata zaidi kucheza vyema na niitwe tena kujiunga na timu siku za usoni. Bado kuna safari ndefu kabla ya Kombe la Dunia na lengo langu halijabadilika.”
Ronaldinho amekuwa akisema kwa muda mrefu sana kwamba ingekuwa vyema kufikisha kilele uchezaji wake bora kwa kuchezea Brazil katika Kombe la Dunia na kushindia mashabiki wa nyumbani taji hilo. Alikosa Kombe la Dunia la 2010 nchini Afrika Kusini na hakuwa akiitwa kujiunga na timu hiyo ya taifa mara nyingi tangu wakati huo, lakini hali ilibadilika Scolari aliporejea mwaka jana na kumjumuisha tena.
Ronaldinho alianza kwenye timu ya Scolari Brazil iliposhinda Kombe la Dunia 2002 nchini Korea Kusini na Japan, na kocha huyo alisema majuzi kuwa anatarajia Ronaldinho kuwa kiongozi wa timu yake.
Ingawa Ronaldinho hakung’ara sana alipochezea timu ya taifa mwaka huu, amecheza vyema sana katika klabu ya Brazil ya Atletico Mineiro, na kujilimbikizia pongezi nchini humo na ni wachache sana waliotarajia aachwe nje.
“Nadhani hili lilishangaza wengi sana kutokana na jinsi timu yangu inavyocheza vyema na kwa kuwa ninafana sana kwa sasa,” akasema.
Scolari alisema sana sana angechagua kati ya Ronaldinho na Kaka kushiriki Kombe la Confederations, na kusema hadharani kwamba Ronaldinho alikuwa katika nafasi bora zaidi lakini hakuna yeyote kati ya vigogo hao aliyeteuliwa.
Ronaldinho na wachezaji wengine wa Brazil walizomewa na takriban mashabiki 50 000 timu hiyo ilipotoka sare ya 2-2 nyumbani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Chile nyumbani mwezi uliopita, lakini alijikwamua na kuiwezesha Atletico Mineiro kufika robo fainali ya Copa Libertadores siku chache tu kabla ya Scolari kutangaza kikosi chake cha Kombe la Confederations.
"Ana ujuzi mwingi na amepitia mengi katika maisha yake ya uchezaji, hivyo anaweza kujikwamua kutoka kwa hili,” alisema mchezaji mwenzake katika Atletico Mineiro, Jo alipoongoea na wanahabari. “Hasikitishwi sana na hatua ya kutojumuishwa kikosini.”
Scolari hakueleza sababu ya kumwacha nje Ronaldinho, na alisema tu kwamba alifanya maamuzi aliyodhani yalifaa zaidi timu.
Vyombo vya habari nchini Brazil zilisema huenda Scolari alikasirishwa na hali kwamba Ronaldinho alichelewa kujiunga na timu hiyo kabla ya mechi dhidi ya Chile, madai ambayo mchezaji huyo alipuuzilia mbali, akisema ingawa alifika katika hoteli iliyotumiwa na timu baada ya wachezaji wengine alifika kabla ya muda uliowekwa na timu hiyo wa kufika. Naibu Carlos Alberto Parreira pia alipuuzilia mbali kisa hicho wakati huo.
Share this article :

Post a Comment

 
thanx to : my family | bongoclan | shebby.c
Copyright © 2011. BONGODASH - All Rights Reserved
imetengenezwa na blogdesinerimepigwa chapa na mchakato
Proudly powered by Blogger